MUDA uliopo kwa sasa katika mapumziko ni kufanya kazi kubwa kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi zijazo huku kila mchezaji akifanya tathimini ya kile ambacho alikifanya uwanjani.
Bado vita ni kubwa kwenye upande wa timu ambazo zinasaka ushindi hilo lipo wazi na litaendelea kuwa hivyo pale ligi itakaporejea kwa mara nyingine tena.
Licha ya kila mmoja kuwa na mtazamo wake ila ukweli upo wazi kila timu inafanya kazi yake kwa umakini kukamilisha majukumu yake na hili ni muhimu na linapaswa kuwa endelevu.
Wakati tunaanza msimu tuliongea kuhusu kila timu kufanya kazi kwa juhudi kwenye mechi zote ambazo watacheza bila kujali kwamba ni mzunguko wa kwanza ama la.
Kwenye mechi ambazo zinachezwa ni muhimu kwa kila mchezaji kufanya kweli uwanjani na muda ni sasa kwa kila mchezaji kufanya kweli kusaka ushindi ndani ya dakika 90.
Inawezekana kupata ushindi kwenye mechi hizi zilizobaki na kuondoka pale ambapo timu ilikuwa ipo katika nafasi mbaya na kufanikisha malengo ya kubaki kwenye ligi.
Umuhimu kwenye mechi zilizopo kwa kila mmoja kufanya kazi kubwa ndani ya uwanja na inawezekana kufanya vizuri kwenye kutafuta ushindi.
Kuna Kombe la Shirikisho pia haya ni mashindano makubwa na yenye ushindani mkubwa huku pia unahitajika ushindani wa kweli na umakini kwenye kutimiza majukumu.
Kila hatua ni muhimu kufanya maandalizi mazuri na inawezekana katika kufanya kweli jambo la msingi ni kupanga mipango kwa umakini kitaifa na kimataifa.
Kila mmoja anapenda kuona timu inapata matokeo chanya na haya yote yanategemea maandalizi ambayo yatafanyika.
Wachezaji na benchi la ufundi ni muda wa kuzidi kushirikiana kwa kila mmoja kufanya kazi kwa ushirikiano katika kutafuta matokeo.
Ipo wazi kwamba wapo ambao kwa sasa wanatambua hawakupata nafasi kwenye mechi zilizopita kutokana na sababu mbalimbali.
Pia rai yangu kwa wachezaji kuongeza umakini kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa mchezaji mwenzake na hii itaongeza nguvu na afya kwa wachezaji kuanza kwa umakini uwanjani.
Imekuwa ikitokea wachezaji kuumia kwenye mechi za ushindani kisha wanakuwa nje kwa muda mrefu wakipambania afya zao.
Hivyo kwa muda uliopo sasa ni muhimu kila mchezaji kuhakikisha kwamba anakuwa balozi mzuri kwa afya ya mchezaji wenzake uwanjani.
Kila la kheri wachezaji kwenye mechi zinazofuata muhimu kuongeza ulinzi ili kuwa imara katika mechi za ushindani na inawezekana kila moja kufanya kazi kubwa kulindana ndani ya uwanja kutokana na kufanya kazi kubwa kusaka ushindi.
Muda uliopo ni sasa kwa kila mchezaji kuongeza umakini na kufanya kazi kubwa kwa ajili ya wakati ujao na inawezekana ikiwa kila mmoja anakuwa kwenye ubora wake.