AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amepiga mkwara mzito kwa kusema kuwa washambuliaji waliosajiliwa watafunga mabao mengi kwelikweli.
Ipo wazi kwamba Simba imeachana na Moses Phiri na mshambuliaji wao namba moja Jean Baleke kwenye dirisha dogo la usajili.
Nyota wapya waliosajiliwa kwa upande wa ushambuliaji ni Pa Jobe na Fred Michael.
Ally amesema kuwa wanatambua kwamba wachezaji ambao wamepewa Thank You walikuwa na mchango mkubwa lakini hakuna namna ya kufanya zaidi ya kujipanga kwa wakati ujao.
“Kwa wachezaji wetu wapya ambao ni washambuliaji kwa kweli tutashangilia mabao kwelikweli kwani ni watu haswa wa kazi, tusubiri na tuone.
“Wale ambao tumeachana nao ni wachezaji wazuri lakini hakuna namna tunawatakia kila la kheri kwenye changamoto mpya,”.