MBWANA Samatta nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Misri ni kipimo tosha katika kuelekea mashindano ya AFCON 2023.
Ikumbukwe kwamba Januari 7 2024 timu ya taifa ya Tanzania ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri baada ya dakika 90 ubao ulisoma, Tanzania 0-2 Misri.
Trezeguet alifunga bao la ufunguzi dakika ya 32 na bao la pili lilifungwa na Mohamed Salah dakika ya 73.
Samatta amesema: “Ulikuwa ni mchezo mzuri na wenye ushindani mkubwa kwa kuwa wapinzani wetu ni timu nzuri. Kucheza na timu ya Misri kwetu ni kipimo tosha kuelekea mechi za AFCON hasa ukizingatia Misri ina uzoefu na wachezaji wazuri,”.