MASTAA YANGA WAPEWA ONYO

MASTAA wa Yanga ambao walifunga 2023 kwa kujenga ushikaji na benchi kwenye mechi za Ligi Kuu Bara wamepewa onyo na benchi la ufundi kuhakikisha kwamba wanatumia vema nafasi watakazopewa.

Ipo wazi kwamba Skudu Makudubela, Cripin Ngushi, Denis Nkane, Jesus Moloko, Jonas Mkude, Aboutwalib Mshery, Kibwana Shomari hawakuwa na nafasi ya kuanza mara kwa mara kikosi cha kwanza kwenye mechi za ligi na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 Yanga ikiwa inashiriki Mapinduzi Cup 2024 nyota hao walianza kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri, Desemba 31 2023 ambapo Ngushi alifunga mabao mawili, Skudu, Kibwana na Clemet Mzize walifunga bao mojamoja kwenye ushindi wa mabao 5-0.

Mussa Ndaw, Kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa ni muhimu kwa wachezaji wanaopata nafasi kwa sasa kuzitumia vizuri ili kuwa imara kwenye mechi zijazo za mashindano kitaifa na kimataifa.

Unaona kwa sasa kuna wachezaji wengi ambao hawapo hapa kwa kuwa wapo kwenye majukumu ya timu ya taifa, Aziz KI, Djigui Diarra na wengine hivyo ni muda wa Ngushi, Kibwana na wengine kuzitumia nafasi hizi kwa umakini.

Tuliwaona kwenye mchezo wetu wa kwanza namna ambavyo walionyesha uwezo mkubwa hilo ni muhimu kuwa endelevu na tunaamini kwamba watazidi kuwa imara kwenye mashindano haya na watapata nafasi kwenye mechi nyingine pia,”.