BOBAN Zirintusa, mshambuliaji wa Mtibwa Sugar ni miongoni mwa mastaa waliosepa na mpira baada ya kufunga hat trick katika mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Aliweza kufanya hivyo Desemba 15 wakati timu ya Mtibwa Sugar ilipotoa dozi ya kifurushi cha wiki kwa Tunduma United ambapo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mtibwa Sugar 7-1 Tunduma United.
Alifunga mabao matatu dk 11,36 na dk 53 mengine yalifungwa na Makang’a dk 16,Makarai dk 48,Mkele dk 75 na Abobakhari dk 90 na Isaya kwa Tunduma dk 57 na kuwafanya waweze kusonga mbele raundi ya nne Kombe la Shirikisho.
Mshambuliaji mwingine ambaye alifunga hat trick kwenye Kombe la Shirikisho ni Heritier Makambo ambaye alifanya hivyo mbele ya Ihefu ambapo timu ya Yanga ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Mkapa.