SHABIKI WA SIMBA, MAN U ASHINDA MILIONI 173 ZA M-Bet

SHABIKI wa Klabu ya Simba na timu ya Manchester United ya England Seif Babu amefunga droo ya Perfect12 ya kampuni ya M-Bet kibabe baada ya kushinda Sh 173,056,020 kwa kubashiri matokeo ya mechi 12 za ligi mbalimbai duniani kiusahihi.

Babu ambaye ni mkazi wa Iringa, alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kubashiri matokeo hayo pamoja na ukweli kuwa kuna baadhi ya timu zimekuwa zikipata matoeko tofauti, tena ya kushangaza.

Mshindi huyo alifunguliwa akaunti na kuweka fedha hizo kwenye benki ya CRDB ambao inashikiana na M-Bet.

Alisema kuwa michezo mingi ya Ligi za mpira wa miguu imekuwa na matokeo ambayo  huwezi kutarajia na kupata changamoto kubwa wakati wa kukamilisha mkeka wake.

“Nimebashiri kwa miezi kadhaa na nimekuwa nikaribia kushinda, unapokosa unatakiwa usikate tamaa, hivyo nilipopigiwa simu kuwa nimeshinda, niliamini kuwa mimi ni mshindi kwani mkeka wa M-Bet na odds zake ni za uhakika na nimeshuhudia washindi mbalimbali wakizawadiwa fedha, hii ni faraja kubwa sana kwangu,” alisema Babu ambaye alivaa kininja kwa sababu za usalama.

Alisema kuwa yeye ni mfanyabiashara ndogo ndogo na atatumia fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza biashara yake na nyingine kuwekeza katika miradi mingine.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa Babu anakuwa mshindi wa tano mwaka huu kushinda droo ya Perfect12 na kuifanya kampuni hiyo kutumia zaidi ya Sh 880 milioni kuzawadia washindi mbalimbali mwaka huu.

Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa ambao wamefaidika na  mwaka huu ambao unafikia ukingoni.

“Tumetoa washindi wengi mpaka sasa ambao wamejishindia mamilioni ya fedha na kuweza kubadili maisha yao ya kila siku. Napenda kuwaambia mashabiki wa soka kuwa kubashiri siyo ajira, ila ni burundani na nawaomab kuzingatia hilo,” alisema Mushi.

Wakati huo huo, mshindi huyo alipewa elimu ya matumizi mazuri ya fedha na benki ya CRDB chini ya meneja wateja wa awali na wa kati, Amina Mawona.

Mawona alisema kuwa CRDB inatoa firsa ya uwekezaji kwa wateja wao kwa kuwapa elimu ili kuwezeka katika miradi ambayo inaleta tija.

Mshindi wa Sh milioni 173 wa mchezo wa kubashiri wa Perfect12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Seif Babu ( katikati) akiwa kayika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania Allen Mushi (wa kwanza kushoto) na Meneja wa wateja awali na wa kati wa benki ya CRDB, Amina Mawona.