Al Ahly imefuzu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu kufuatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Al-Ittihad ya Saudi Arabia kwenye mchezo wa robo fainali.
FT: Al Ahly ?? 3-1 ?? Al Ittihad
⚽ Maâloul (P) 21’
⚽ E lShahat 59’
⚽ Ashour 62’
Al Ahly itachuana na vigogo wa Brazil, Fluminense ambao ni Mabingwa wa Amerika ya Kusini (CONMEBOL Libertadores Champions) kwenye hatua ya nusu fainali.
Ikumbukwe Al Ittihad imesheheni nyota ambao ni washindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, N’golo Kante (Chelsea), Fabinho (Liverpool) na Karim Benzema (Real Madrid) ambaye pia ni mshindi wa Ballon d’or.