MASTAA HAWA YANGA HABARI NYINGINE KIMATAIFA

MASTAA wa Miguel Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi wakiongozwa na Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli, Kennedy Musonda ni habari nyingine.

Nyota hao ushirikiano wao umekuwa na matokeo chanya katika mechi mbili zilizopita za Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo ni dakika 180 nyumbani na ugenini.

Katika mchezo dhidi ya Al Ahly uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Pacome alipachika bao la kuweka usawa wakifungana 1-1 ilikuwa dakika ya 90 akitumia pasi ya mshikaji wake Kennedy Musonda.

Pacome alirejea kambani kwa mara nyingine ugenini walipovaana na Medeama alipoachika bao la kuweka usawa dakika ya 36 wakigawana pointi mojamoja ugenini katika mchezo wa tatu.

Maxi licha ya kukwama kufunga wala kutoa pasi ya bao dhidi ya Medeama alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 20 na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 41 kutokana na harakati za kuokoa hatari.

Kiungo Khalid Aucho kwenye eneo la kiungo mkabaji mechi zote tatu alikomba dakika zote 90 mazima zinazomfanya kuyeyusha dakika 270 kimataifa.