KLABU ya Kagera Sugar inayotumia Uwanja wa Kaitaba kwa mechi zake za nyumbani hasira zake kwa sasa ni kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Simba.
Kagera Sugar inatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Simba Desemba 15 katika msako wa pointi tatu muhimu.
Desemba 9 Kagera Sugar walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ukisoma Coastal Union 1-0 Kagera Sugar na kuacha pointi tatu ugenini.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa ambapo Simba haijapata ushindi kwenye mchezo wake uliopita wa ligi ilipogawana pointi mojamoja na Namungo kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Marwa Chamberi, Kocha msaidizi wa Kagera Sugar amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo jambo ambalo linawafanya wafanye maandalizi kwa kila mchezo.
“Ushindani ni mkubwa hilo tunalitambua hivyo tunafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi zetu zote zilizopo mbele. Wachezaji wapo tayari kwa ajili ya kuona tunapata pointi tatu,”.