>

YANGA YAVUNA POINTI MOJA UGENINI

KATIKA mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika wawakilishi wa Tanzania, Yanga wakiwa ugenini wamevuna pointi moja.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Baba Yara Sports umesoma Medeama 1-1 Yanga ambapo mabao yote yamefungwa kipindi cha kwanza katika dakika 45 za mwanzo.

Medeama walianza kupata bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 27 kupitia kwa Jonathan likawekwa usawa na Pacome Zouzoua dakika ya 36.

Kwenye mchezo wa leo Miguel Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga alianza na washambuliaji wawili Mzize na Musonda na kwenye upande wa viungo Maxi Nzengeli, Pacome walianza huku kwa ukabaji ni Khalid Aucho.

Katika kundi D Desemba 8 hakuna mbabe aliyesepa na pointi tatu kwa kuwa Al Ahly 0-0 CR Belouzdad ambao wote wapo kundi D.