NI Rais wa Yanga SC, Hersi Said amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Vilabu barani Afrika (African Clubs Association – ACA), katika uchaguzi uliofanyika leo nchini Misri.
Hersi atasaidiwa na makamu wenyeviti wawili ambao ni Jessica Motaung wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na Paul Bassey kutoka Akwa United ya Nigeria.