TAIFA STARS KUPOTEZA DHIDI YA MOROCCO UBORA UMEAMUA

MCHEZO uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Novemba 21 2023 umeacha maumivu kwa mashabiki kwa kushuhudia timu pendwa ikipoteza.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Tanzania 0-2 Morocco huku nyota Dismas akiingia kwenye orodha ya wachezaji walioonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Ni mabao ya Hakim Ziyechi dakika ya 28 na Lusajo Mwaikenda dakika ya 54 alijifunga kwenye harakati za kuokoa hatari langoni mwa Stars.

Ukiangalia haraka unaweza kuona ni kama mabao mawili mepesi hivi lakini ni ubora umeamua hivyo bado kuna nafasi ya kufanyia kazi makosa kwa ajili ya mechi zinazofuata.

Kimfumo Stars walikaa vizuri lakini makosa machache ya utekelezaji mfumo wenyewe ni sababu ya kupoteza mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Ikumbukwe kwamba ilikuwa ni mechi ya timu bora namba moja Afrika walionyesha ukubwa wao katika Kombe la Dunia kwa kuzipa ugumu timu kubwa lakini yote ni maisha ya mpira.