MAANDALIZI MAKINI YANAHITAJIKA KUPATA MATOKEO KWA MKAPA

KIKUBWA ambacho kinatakiwa kwa wachezaji kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi ni kulindana ndani ya dakika zote 90.

Presha ni kubwa kwa kila upande hilo lipo wazi ila kuna ulazima wa kila mmoja kuwa makini kwenye mchezo ambao unasubiriwa kwa shauku kubwa.

Mchezo wa Simba na Yanga kila Mtanzania anapenda kuona burudani. Kuonyesha ubora wa ligi ya Tanzania taswira yake inapaswa kuchorwa kwa umakini na sio kwa mkaa hilo litakuwa ni doa.

Kila mchezaji anapaswa kuwa mlinzi wa mchezaji mwenzake dakika zote Uwanja wa Mkapa. Kuchezeana faulo ambazo hazina nafasi kusipewe nafasi kwenye mchezo husika.

Muda ni sasa na kila mmoja ana nafasi kubwa kupata ushindi akitumia makosa ya mpinzani wake. Hakuna ambaye hapendi kupata matokeo mazuri lakini mipango lazima iwe makini.

Kwa muda ambao umebaki ni lazima wachezaji kujituma katika kutimiza majukumu yao. Inawezekana kuwa mchezo wenye ubora ikiwa kila timu itatimiza majukumu kwa wakati na wachezaji wakichezeana faulo za hovyo ule mvuto wa mchezo utapotea.

Mpira sio vita kwa wapinzani kupaniana ndani ya uwanja bali mbinu zinatakiwa kutawala kwenye mchezo husika. Burudani kwa mashabiki ni kuona mpira ukipita kwenye njia zake.

Matokeo mazuri yatapatikana kwa timu itakayokuwa makini kutumia makosa ya mpinzani wake na hiyo itakuwa ni kwa timu zote mbili.

Wakati ni sasa kufanyia kazi makosa kwenye mechi zilizopita ili kupata matokeo mazuri baada ya mchezo kukamilika.