WAKIJIANDAA na mchezo wao wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu wa Simba, Robert Oliveira ‘Robertinho’ amechimba mkwara mzito kuwa wametumia uzito wa michezo yao miwili ya AFL, dhidi ya Al Ahly kujiandaa na uzito wa mchezo wa kesho.
Simba wanaingia katika mchezo huu wakiwa wamecheza mchezo mmoja tu wa Ligi Kuu Bara baada ya kutoka kwenye ratiba ya mashindano ya African Football League ambayo waliishia robo fainali baada ya matokeo ya jumla ya sare ya mabao 3-3.
Robertinho amesema: “Ni kweli tunatarajia mchezo mgumu sana mbele ya Yanga kutokana na ubora wa kikosi chao, lakini kama kikosi tunajivunia ubora wa maandalizi yetu kuelekea mchezo huu.
“Tunatambua namna wapinzani wetu walivyo na utakuwa ni mchezo mgumu lakini tupo tayari kwa ajili ya kupata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu,”.
Miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wapo tayari kwa mchezo wa kesho ni Luis Miquissone, Clatous Chama, John Bocco, Jean Baleke.