KIVUMBI TUPU TATU BORA UFUNGAJI

KIVUMBI tupu ndani ya tatu bora ya ufungaji kutokana na mastaa waliopo hapo kuwa na rekodi zao zinazovutia namna wanavyofunga na kukamilisha majukumu yao.

Ni Aziz KI wa Yanga huyu ni namba moja kwenye utupiaji akiwa na mabao sita, Jean Baleke yupo zake ndani ya Simba mabao matano na Feisal Salum, (Fei Toto) yupo Azam FC yupo zake ndani ya Azam FC.

Rekodi zinaonyesha kuwa mastaa wote waliopo ndani ya tatu bora wana hat trick kibindoni, alianza Feisal Salum ilikuwa dhidi ya Tabora United, mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Bao la nne Fei Toto alifunga dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga likiwa ni bao pekee lililoipa pointi tatu timu hiyo ugenini ilikuwa dakika ya 45.

Baleke hat trick yake alitupia Uwanja wa Uhuru ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, mabao yake hayo matatu yalitosha kuipa pointi tatu Simba na yeye alifikisha jumla ya mabao matano kibindoni.

Aziz KI ni dhidi ya Azam FC alifunga hat trick wakati Yanga ikikomba pointi tatu mazima ikiwa nyumbani yeye akifikisha jumla ya mabao sita.Hat trick tatu zilizofungwa kila timu ilikuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.