MASHABIKI wa Simba wameweka wazi kuwa licha ya kutolewa na Al Ahly kwenye hatua ya robo fainali African Football League wamekufa kiume. Timu ya Simba chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1. Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-2 Al Ahly. Jumla ni mabao 3-3 Al Ahly inasonga mbele kwa faida ya mabao mengi ugenini Uwanja wa Mkapa.