WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano mapya ya African Football League safari yao imegota mwisho baada ya kuondolewa na Al Ahly waliopata faida ya kuwa na mabao mengi ugenini.
Mchezo wa robo fainai ya pili ambao umechezwa nchini Misri, Oktoba 24 ubao umesoma Al Ahly 1-1 Simba.
Bao la Simba limefungwa na Sadio Kanoute dakika ya 69 na lile la Al Ahly limefungwa na Karhaba dakika ya 76.
Mwisho ni Al Ahly 1-1 Simba (Agg: 3-3) Safari imegota mwisho wakiambulia bao moja ugenini na wao Al Ahly waliambulia mabao mawili ugenini.