NYOTA Feisal Salum (Fei Toto) ana balaa huyo ndani ya uwanja kwa kuwa namba moja kwenye utupiaji wa mabao ndani ya Azam FC.
Ndani ya Ligi Kuu Bara katupia mabao manne ambapo ni mchezaji wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi alipofunga kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Azam Complex.
Alianza kucheka na nyavu Agosti 16, 2023 katika dimba la Azam Complex, Chamazi na kufanikiwa kufunga mabao matatu ndani ya dakika 13 tu za mchezo huo dhidi ya Tabora United.
Ni Oktoba 6, 2023 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Mkwakwani Tanga nyota huyo alipachika bao lake la nne.
Kwenye mchezo huo alipachika bao hilo kipindi cha kwanza akitumia makosa ya safu ya ulinzi ya timu hiyo katika harakati za kuokoa hatari langoni.
Tangu atue Azam FC mwanzoni mwa msimu huu akitokea Yanga, Feisal amekutana na Wananchi kwenye mchezo mmoja wa Ngao ya Jamii uliopigwa kule Tanga na vijana hao wa Chamazi kupoteza kwa jumla ya mabao 2-0.