HIVI NDIVYO MTU WA KAZI JOB ALIVYOMTULIZA CHE MALONE

MWAMBA Dickson Job beki wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga amemtuliza mazima mwamba Che Malone kwenye kuzuia hatari katika lango hilo ndani ya mechi tano ambazo ni dakika 450.

Job ni chaguo la kwanza la kwanza chini ya Miguel Gamondi anashikilia rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga bao ndani ya Yanga msimu wa 2023/24 ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya KMC dakika ya 16.

Mbali na kufunga nyota huyo kampoteza beki wa Simba Che Malone kwenye idadi ya mabao ya kufungwa katika mechi hizo tano ambazo walicheza kwa msimu huu.

Yanga imeokota nyavuni mabao mawili pekee ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Ihefu uliochezwa Uwanja wa Highland Estate baada ya dakika 90 ubao ulisoma Ihefu 2-1 Yanga.

Kwa upande wa Simba ukuta wao unaoongozwa na Che Malone kwa sasa ulitunguliwa mabao manne huku beki huyo akiwa hajapata zali la kufunga.

Mchezo wa kwanza msimu wa 2023/24 ni mabao mawili alishuhudia yakiwa ndani ya nyavu na mechi mbili za ugenini mfululizo waliokota bao mojamoja, dhidi ya Tanzania Prisons, Singida Fountain Gate.