NIDHAMU NGUZO KUBWA KWA MAFANIKIO

KAZI ni kubwa kwa timu zote kuendelea kufanyia maboresho pale penye upungufu kupitia mechi zilizopita. Tumeona namna ligi ilivyo na ushindani hii ni kubwa na inaonyesha thamani ya ligi yetu ya ndani.

Jambo la msingi ni kuona kunakuwa na mwendelezo mzuri kwa mechi zinazofuata. Ushindani ambao uliopita kwenye mechi za mwanzo kabla ya ligi kusimama unapaswa kuendelea.

Ikiwa hali itakuwa hivyo mpaka mwisho tutapata mshindi ambaye atakuwa amepata zile ladha na chungu za ligi. Uwekezaji uliopo kwa sasa ni mkubwa jambo ambalo linatoa majibu ya kinachopatikana.

Kuanzia kwa wachezaji mpaka benchi la ufundi kila mmoja anaonyesha utofauti wake. Zipo timu ambazo zilikwama kupata ushindi na zipo timu ambazo zilipata ushindi katika mechi zao.

Usisahau kwamba zipo timu ambazo zilifungwa mabao mengi na ambazo zilifungwa mabao machache. Yote haya ni kutokana na maandalizi husika kuelekea mchezo wa ushindani.

Kwa namna ambavyo kila timu inashinda mechi zake inamaanisha kuwa ugenini na nyumbani matokeo yanapatikana. Jambo la msingi kwa kila timu kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mechi zijazo.

Mwanzo wa mechi za mzunguko wa kwanza ni picha ya kule tunakoelekea. Muhimu kwa wachezaji kuwa makini kufuata maelekezo wanayopata kutoka kwenye benchi la ufundi.

Kila idara ni muhimu kuwa imara ili kupata matokeo chanya. Kuanzia safu ya ulinzi na ushambuliaji hapa kuna ulazima wa kutazama mapungufu ambapo yalionekana kwa mechi zilizopita.

Nafasi ambazo zinapatikana kwenye mechi husika ni aghalabu kuipata kwa mara nyingine. Umakini mkubwa kwa safu ya ushambuliaji unaongeza nguvu ya kupata matokeo kwenye mechi zote.

Ikiwa timu itapata matokeo chanya kwenye mchezo husika ni nguvu kuelekea mchezo ujao na inawezekana kushinda. Nidhamu kwenye mazoezi pamoja na mchezo husika ni mwanzo wa kupata matokeo mazuri.

Muda uliopo ni sasa na kila timu ina nafasi ya kupata matokeo chanya. Kila mchezaji anapenda kuona matokeo mazuri yanapatikana na hili halitokei kwa bahati mbaya muhimu ni kuendelea kufanya maandalizi mazuri.

Kuanzia ushambuliaji ni eneo muhimu kwa timu kupata ushindi.Nafasi ambazo watazipata kwenye mchezo husika ni muhimu kuzitumia kupata matokeo mazuri kwenye mchezo husika.

Upande wa ulinzi ni muhimu nao kuangalia idadi ya mabao ambayo waliruhusu kwenye mechi zilizopita. Kuna umuhimu wa kila idara kuwa bora kutengeneza muunganiko mzuri.

Mabao yanayopatikana kupitia safu ya ushambuliaji ni muhimu kulindwa ili kupata huo ushindi. Dakika 90 za kusaka pointi tatu jasho kila kona linavuja kuanzia ushambuliaji mpaka ulinzi.

Kwa timu ambazo hazikuwa na mwendo mzuri kwenye mechi za mwanzo muda uliopo ni sasa kufanyia maboresho makosa yaliyopo kwa ajili ya kupata matokeo kesho.

Hakuna ambacho kinashindikana ikiwa nidhamu itakuwa nguzo kwenye kila mchezo.Dakika 90 za maamuzi haziamuliwa kwa nafasi zinazopatikana pekee bali mpaka namna ya kuukamilisha mchezo husika.

Kila la kheri wachezaji kwenye kutimiza majukumu yenu. Inawezekana na muda uliopo wa kufanyia kazi makosa kwa ajili ya kesho ni sasa.