MCHEZO wa kimataifa wa leo kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni muhimu kupambana kupata matokeo. Kete ngumu na itakuwa na ushindani mkubwa.
Wachezaji ni muda wa kuonyesha thamani ya kile ambacho kipo kwenye miguu yenu. Muda ambao ulipatikana kwa maandalizi unatosha na sasa ni kazi kuonesha ukweli kwenye vitendo.
Nafasi yenu ni kubwa na uwezo mnao kuwapa furaha Watanzania. Hii ni nafasi ya kuonyesha ubora wa kile mlichonacho kilichowapa fursa ya kuwa hapo.
Sudan sio wa kuwabeza, wapo imara nao wanahitaji ushindi. Kupata ushindi kwenye mechi za kirafiki kutaongeaza nguvu ya kujiamini kwenye mechi zijazo. Kuwa ugenini ni faida ikiwa ushindi utapatikana.
Wakati ni sasa kwa kila mchezaji kupambana kwenye dakika 90 kusaka ushindi. Ushirikiano wenu utaleta matokeo mazuri uwanjani. Hilo lipo wazi na nawezekana.
Nidhamu ni msingi kufikia mafanikio kwenye kupata matokeo mazuri. Ipo wazi kuwa wachezaji furaha ni matokeo mazuri kama ilivyo benchi la ufundi.
Ikawe hivyo kwa kuhakikisha mnapunguza makosa na kutumia nafasi ambazo zitapatikana kwenye mchezo wa leo wa kimataifa.
Umuhimu mkubwa wa mchezo huu mbali na kuongeza hali ya kujiamini ni mchezo wa kuongeza pointi kwa taifa kwenye upande wa nafasi za kimataifa.
Iwe ni mechi itakayoleta matokeo chanya na kila mchezaji atakayepata nafasi kujituma kutimiza majukumu yake na inawezekana.