ZIKIWA zimesalia takribani siku nane kabla ya Simba hijacheza dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League, uongozi wa timu hiyo umesema watawaonesha wapinzani wao kwamba Simba ni timu ya aina gani.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, kisha marudiano Oktoba 24, Misri.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally, amesema wana malengo ya kuhakikisha wanakwenda kushindana na sio kushindwa, hivyo wana kila sababu ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ambao ni muhimu kwao kushinda.