Home Sports SIMBA HESABU KUBWA KWA AL AHLY

SIMBA HESABU KUBWA KWA AL AHLY

ZIKIWA zimesalia takribani siku nane kabla ya Simba hijacheza dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya African Football League, uongozi wa timu hiyo umesema watawaonesha wapinzani wao kwamba Simba ni timu ya aina gani.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, kisha marudiano Oktoba 24, Misri.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally, amesema wana malengo ya kuhakikisha wanakwenda kushindana na sio kushindwa, hivyo wana kila sababu ya kupata matokeo mazuri katika mchezo huo ambao ni muhimu kwao kushinda.

“Tunatambua Al Ahly ni wakubwa na ni namba moja kwenye ubora hilo lipo wazi. Sisi tunafanya maandalizi mazuri ili kupata matokeo kwenye mchezo wetu ambao ni muhimu na tunaanzia nyumbani.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuishuhudia timu yao pendwa ikifanya yao tunaamini itakuwa ni siku nzuri na ya burudani kwa kila atakayejitokeza,” amesema.

Previous articleKAZI BADO IPO KWENYE LIGI, MAKOSA YAFANYIWE KAZI
Next articleYANGA WAMEREJEA RELINI HHII NI ISHARA LIGI KUU USHIDANI UTAPANDA