UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa maandalizi ambayo wanafanya kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni mwendelezo wa kurejea kwenye ligi kuendeleza kazi ya kutetea taji lao.
Ipo wazi kuwa msimu wa 2022/23 Yanga ilitwaa taji la Ligi Kuu Bara huku watani zao wa jadi Simba wakigotea nafasi ya pili.
Agosti 23 kikosi cha Yanga kinatarajiwa kutupa kete ya kwanza kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC Uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wao wa kwanza kwenye ligi.
Ikumbukwa kwamba wachezaji wa Yanga Jumapili wametoka kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS Djibout Uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa kimataifa.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma ASAS Djibout 0-2 Yanga na marudio yanatarajiwa kuwa Jumapili ya wiki hii.
, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa kazi inayofanyika ni kukiandaa kikosi kwa ajili ya mechi za ligi na za kimataifa.
“Kikosi kinaandaliwa kwa ajili ya mechi zote zile za kitaifa na kimataifa kulingana na ratiba yetu ilivyo hatuna namna kikubwa ni kujipanga vizuri.
“Tunaamini benchi la ufundi linatambua vema ratiba yetu pamoja na mpangilio kwenye mechi zote ambazo ni muhimu tukitoka kwenye mchezo wa kimataifa tunakweda kwenye mechi za ligi kote tunapambana kupata matokeo chanya,” amesema Kamwe.