KINAWAKA LEO LIGI KUU BARA

HATIMAYE kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinatarajiwa kuanza leo Agosti 2023 kwa baadhi ya mechi kupigwa viwanjani.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 ambapo mabingwa walikuwa ni Yanga tarehe kama ya leo Agosti 15 ligi ilianza na mchezo wa ufunguzi ilikuwa Ihefu 0-1 Ruvu Shooting.

Ihefu timu ya kwanza kuitungua Yanga kwenye ligi inakwenda kufungua pazia tena kwa mara nyingine ikiwa Uwanja wa Highland Estate.

Ni Ihefu itaanza ikiwa nyumbani, Uwanja wa Highland Estate, Mbeya kwa kuwakaribisha Geita Gold.

Timu hiyo inafundishwa na Zuber Katwila ambaye atakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Geita Gold.

Dakika 90 nyingine za moto ni kwenye mchezo wa Namungo dhidi ya JKT Tanzania huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa.

JKT Tanzania ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 itakuwa ugenini ikikaribishwa na Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedrick Kaze ambaye msimu wa 2022/23 alikuwa ndani ya kikosi cha Yanga.

Kete ya tatu inayotarajiwa kuchezwa leo ni Dodoma Jiji hawa watawakaribisha Coastal Union katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Yanga wao ambao ni mabingwa watetezi kete yao ya kwanza itakuwa dhidi ya KMC mchezo unoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex .