KARIBU mgeni mwenyeji apone, ipo hivyo jambo ambalo wamekuja nalo Mashujaa FC kutoka Kigoma kwa kuingia anga za Simba na Yanga.
Ikumbukwe kwamba Mashujaa FC ilipata nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Bara baada ya kuifungashia virago Mbeya City kwenye mchezo wa mtoano hivyo Mbeya City itashiriki Championship msimu wa 2023/24.
Ni Mashujaa Day timu hiyo inakuja nayo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Agosti 12, 2023 kwa kutambulisha wachezaji wapya, uzi mpya na benchi la ufundi.
Timu hiyo tayari imezindua uzi wao mpya kwa ajili ya msimu wa 2023/24 kambi yake ya maandalizi kwa msimu ujao ilikuwa Zanzibar chini ya Kocha Mkuu Mohamed Abdallah (Bares).