YANGA YAMALIZA WIKI KWA BATA

VINARA wa Ligi Kuu Bara, Yanga walimaliza wiki kwa bata kabla ya leo kuanza kuivutia kasi Simba.

Timu hiyi ambayo imekuwa katika mwendo kasi ipo na pointi zake 19 baada ya kucheza mechi 7, imeshinda sita na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Namungo FC.

Desemba 5 wakati Simba ilipokuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Red Arrows wao walikuwa wakila bata batani katika hoteli ya White Sand na hawakutupia jezi zao.

Wachezaji na benchi la ufundi wote walikuwa katika muonekano wa kawaida bila jezi kwa kuendelea kuwa katika furaha kama kawaida.

Leo Desemba 6 maandalizi yanatarajiwa kuanza kuivutia kasi Simba, Desemba 11, Uwanja wa Mkapa.