SIMBA YAANZA KWA USHINDI DHIDI YA POWER DYNAMO

KATIKA kilele cha Simba Day Agosti 6 2023 maelfu ya mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Mkapa wameshuhudia burudani kutoka kwa mastaa wao waliotambulishwa.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Simba 2-0 Power Dynamo ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Mabao ya Simba yamefungwa na Willy Onana dakika ya nne na Fabrince Ngoma dakika ya 75 ya kipindi cha pili.

Kabla ya mchezo wachezaji walipata fursa ya kusalimiana na mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu aliyebainisha wazi kuwa ni muhimu timu zote kwenye mashindano ya kimataifa zikashirikiana.