SIMBA KUREJEA BONGO KUENDELEA NA KAZI

BAADA ya kikosi cha Simba kuweka kambi kwa muda Uturuki, Agosti Mosi safari ya kurejea Dar imeanza ili kuendelea na maandalizi ya mwisho kwa msimu wa 2023/24.

Agosti 6 Simba itakuwa na tamasha la Simba Day lililotanguliwa na watani zao wa jadi Yanga kukamilisha Wiki ya Mwananchi.

Agosti 2 ni Singida Big Day ambayo ni maalumu kwa ajili ya Singida Fountain Gate inayotarajiwa kufanyika Uwanja wa Liti.

Julai 12 kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kiliwasili Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24.

Timu hiyo inatambua kwamba msimu wa 2022/23 ilikosa ubingwa na Yanga walitwaa ubingwa wa ligi hivyo wanapambana kufikia malengo yao.

Miongoni mwa nyota ambao walikuwa kwenye kikosi hicho ni Jean Baleke, Kibu Dennis, David Kameta, Clatous Chama, Moses Phiri, John Bocco.

Chama alikuwa anatajwa kuibukia kwa watani wa jadi Yanga na mwisho wa siku uongozi wa Simba ulimalizana naye kuhusu masuala ya maboresho ya mkataba wake.