VIDEO:SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA KIPA MPYA/ ALIUMIA MAZOEZINI

KIPA mpya wa Simba Luis Jefferson anatajwa kupata maumivu kwenye mazoezi Uturuki ikiwa ni muda mfupi tangu atambulishwe.
DR Shabiki wa Simba amebainisha kuhusu suala la mchezaji huyo ambaye hajapata fursa ya kucheza kwenye ligi ya Tanzania inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Ikumbukwe kwamba ni Yanga ambao ni mabingwa wa msimu wa 2022/23 huku Simba ikigotea nafasi ya pili kwenye msimamo. Yanga na Simba zina kazi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mbali na Yanga pia Singida Fountain Gate nayo ipo kwenye orodha ya timu za kimataifa na Azam FC kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.