Home Uncategorized WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA SIO KINYONGE

WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA SIO KINYONGE

KLABU ya Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ina kibarua cha kuipeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa.

Ni katika Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga itakuwa na kazi ya kupeperusha bendera ya Tanzania.

Katika hatua ya awali Yanga inatarajiwa kumenyana na Association Sportive d’Ali Sabieh Djibouti Télécom ambayo haipo kinyonge uwanjani.

Wapinzani wa Yanga ni klabu kutoka Djibouti inashiriki kwenye ligi kuu ya Djibouti Premier League.

Klabu ya As Ali Sabieh imeanzishwa mwaka 1991 na inamiliki uwanja wa El Hadj Hassan Gouled Aptidon.

Uwanja wa wapinzani wa Yanga kimataifa una  uwezo wa kuingiza mashabiki 20,000 .

Asas wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya ndani “Djibouti Premier League” mara saba na Djibouti Cup mara tatu ndio klabu iliyofanikiwa zaidi nchini humo.

Yanga ina kazi ya kupata ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Previous articleVIDEO:SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA KIPA MPYA/ ALIUMIA MAZOEZINI
Next articleMAXI, SKUDU WABEBESHWA MZIGO YANGA, LUIS AMPA MZUKA ROB