HAPA UJANJA WA AZIZ KI UMEJIFICHA

MGUU wenye nguvu kwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Aziz KI ni ule wa kushoto unaompa maujanja ya kuwapa maumivu makipa ndani ya Ligi Kuu Bara.

Msimu wa 2022/23 ameutumia kufunga mabao 9 kwenye ligi ndani ya Yanga na kutoa pasi tano za mabao.

Timu yake ya kwanza kuifunga ilikuwa ni Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa ligi.

Katika mchezo huo Aziz KI alitokea benchi alipotambulishwa na Nasreddine Nabi aliyekuwa kocha wa Yanga.

Mbali na kuifunga Mtibwa Sugar Aziz KI bao moja aliwatungua watani zake wa jadi Simba kwenye mchezo wa ligi.

Ni pigo huru maeneo ambayo Bernard Morrison alipokuwa ndani ya Yanga aliwahi kumtungua Aishi Manula naye akarudia kwa kipa yuleyule namba moja wa Simba.