BAADA ya Aziz KI kutoka ASEC Mimosas amefungua njia kwa wachezaji wengine kutoka hapo kuja kwenye ligi ya Bongo baada ya kujiunga na Yanga.
Wakati mzuri kwao wanauza na maisha yanaendelea bila kuyumba jambo ambalo ni somo kwa timu za Bongo.
Kuna baadhi ya timu zikiuza mchezaji mmoja kila kitu kinakuwa kipya na wanapambana kurejea kwenye ubora kwa muda.
Ni wakati wa kujifunza kwa wakati mwingine kuwa bora kila wakati.
Kuna nyota wengine wanafuatiliwa na Simba na Yanga ambao wanacheza ASEC Mimosas.
Simba haijamaliza suala la usajili na ipo sokoni ikisaka saini ya mshambuliaji, kiungo na kipa huku asilimia kubwa hivi karibuni watatambulisha kiungo mwingine.
Yanga nao wanapambana kusaka saini ya mshambuliaji wakiwa kwenye hesabu za mwisho kumtambulisha kiungo na winga.
Bado Yanga na Simba hazijamaliza usajili kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023/24 hivyo lolote linaweza kutokea.