SAMATTA KWENYE CHANGAMOTO MPYA

MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta ambaye akipata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars hupewa kitambaa cha unahodha ameweka wazi kuwa ana furahi kuanza kupata changamoto mpya.

Nyota huyo atakuwa ndani ya Paok kwa ajili ya kupata changamoto mpya ndani ya msimu wa 2023/24.

“Hello Paok ninafurahi kuwa hapa nina amini kwamba tutafanya kazi kubwa kwa ushirikiano nipo tayari kwa ajili ya hilo na ni furaha kwangu kuwa pamoja nanyi,”.

Samatta ametoa shukrani kwa timu ambazo amepitia ikiwa ni pamoja na KRC Genk pamoja na Fenerbahce za Ubelgiji.

Nyota huyo ni Mtanzania wa kwanza kucheza ndani ya Ligi Kuu England alipojiunga na Aston Villa kwa Afrika alicheza TP Mazembe na Simba kwenye soka la ushindani.

Kila la kheri Samatta kwenye changamoto mpya