NYOTA Deus Kaseke ni miongoni mwa wale watakaokuwa kwenye kikosi cha Singida Fountain Gate kwa ajili maandalizi ya msimu wa 2023/24.
Timu hiyo kambi yake itakuwa Arusha baada ya mpango wa kuelekea Tunisia kusitishwa.
Kaseke ni Legend ndani ya timu hiyo kutokana na uwezo wake kwenye eneo la kiungo na aliibuka hapo akitokea Yanga.
Mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2023/24 utakuwa ni wa Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali dhidi ya Simba.
Ni Tanga, Uwanja wa Mkwakwani mchezo huo unatarajiwa kuchezwa na mshindi wa mchezo huo atakutana na mshindi wa fainali kati ya Azam FC dhidi ya Yanga.