JEMBE LA KAZI LINATUA YANGA

GIFT Fred kutoka SC Villa ya Uganda anatajwa kuwa kwenye hesabu za mabosi wa Yanga.

Yanga ipo kwenye mpango wa kuboresha timu hiyo kwa ajili ya msimu wa 2023/24.

Ni Nikson Kibabage huyu ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga na wengine wanafuata.

Mwamba huyu ni beki ambaye dili lake likikamilika atakuja kuongeza nguvu kwenye eneo la ulinzi.