Skip to content
KILA mmoja wakati wa usajili anaonekana kuwa na furaha akivutia upande wake kuwa usajili utakuwa bora na imara.
Sio Simba, Yanga, Geita Gold mpaka Mtibwa Sugar neno ni moja watafanya usajili mzuri utakaoleta matokeo chanya.
Singida Fountain Gate FC hawa wanashiriki mashindano ya kimataifa kama ilivyo Azam FC ambao wameanza kutambulisha mashine zao za kazi.
Wote wanatambua kwamba Yanga ametwaa ubingwa na malengo ni kuutetea kwa msimu ujao huku wao malengo yao ikiwa ni kutibua ubingwa huo.
KMC hawakuwa na mwendo mzuri na kugotea kucheza mchezo wa mtoano nao wana kazi ya kufanya msimu ujao.
Ipo wazi kuwa baada ya dirisha la usajili kufunguliwa kila mmoja amekuwa akifanya kazi yake kupambania kile ambacho anahitaji.
Iwe hivyo kwa namna ambavyo kila kiongozi anafurahi kuwa watafanya usajili mzuri wataleta wachezaji makini hata wakati wa matokeo.
Kila timu ni muda wa kufanya maboresho kwenye timu zao hilo ni jukumu muhimu na pale ambapo watafanya maboresho itaongeza uimara wa timu zao.
Ikiwa kila mmoja kwa sasa anapambana kuonyesha furaha kwa mashabiki hilo linaongeza nguvu kwenye kupambania malengo yao.
Kila mmoja anafurahi kuambiwa watafanya usajili mzuri na wachezaji wenye ubora ndani ya timu basi furaha hiyo idumu muda wote.
Ukweli ni kwamba muda wa kufanya kazi ya usajili ni sasa na kila timu ni muhimu kuendeleza furaha mpaka muda wa kusaka matokeo.
Mwisho wa siku kazi kubwa itakuwa ni kutazama matokeo uwanjani hilo litaongeza furaha na kuongeza maumivu yale ambayo watavuna.
Muda wa mavuno unakuja lakini kwa sasa ni muda wa kuanza kupambana kujenga ile furaha ambayo inatengenezwa kwa sasa kwa viongozi na promo zao.
Porojo hazichezi ni wachezaji na wale ambao watapata nafasi kwenye timu zao ni muhimu kupambana kutimiza majukumu yao