KAIZER CHIEFS YAPATA KOCHA MPYA, NAI IMEBUMA

KLABU ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imemtangaza rasmi Molefi Ntseki kuwa ndiye kocha wao mkuu kwenye timu hiyo.

Kutokana na hatua hiyo, ni wazi kwamba klabu hiyo ya Kaizer Chiefs imeamua kuachanana na mpango wake wa kumpa kazi Nassredine Nabi ambaye alikuwa kocha mkuu wa Klabu ya Yanga.

Nabi alikuwa ndani ya Yanga kwa msimu uliopita na alifanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Kutokana na maamuzi ya Kaizer Chiefs, kumekuwa na tetesi mbalimbali ambazo zinaeleza kwamba Kaizer Chiefs wameamua kuachana na kocha huyo ambaye ni raia wa Tunisia baada ya kushindwa kuafikiana hususani katika suala linalohusiana na benchi la ufundi.

Katika suala hilo, kocha Nabi aliomba kwenda na watu wake watatu huku Kaizer Chiefs wakisisitiza kwamba aende na mtu mmoja na kisha wengine atawakuta kule kule.

Lakini kutokana na uwezo wa Nabi ipo wazi kuwa atapata timu hivi karibuni.