NGOJANGOJA huumiza tumbo imekuwa hivyo na itabaki kuwa hivyo kwa kile ambacho kinapatikana ni lazima kugawana kwa haki bila upendeleo.
Mawazo mazuri ambayo yanakusanywa ni muhimu kufanyiwa kazi hasa ukizingatia kila kitu ambacho kinafanyika kinaanzia kwenye mpango kazi wa fikra.
Ipo hivi Wanachama wa Yanga wanatarajia kufanya mkutano mkuu ambao huo upo kwa mujibu wa katiba hakika kwa kulitambua hili na kulifuata pongezi wanastahili.
Mkutano wa Yanga uwe na matokeo mazuri kwa yale ambayo yatajadiliwa kwa marefu na mapana na Imani kubwa ni kwa wahusika wale waliokidhi vigezo kuhudhuria.
Zile ngonjera ndefu na porojo kwenye mkutano zinapaswa kuepukwa na badala yake msingi uwe kwenye kujenga hoja zenye mashiko na manufaa kwa ajili ya timu na taifa kiujumla.
Unapozungumzia umoja na mafanikio huwa havikubali kuachana hata hatua moja kila sehemu vinagandana hapo ni muhimu kuangalia pale penye mapungufu ili kufanyia kazi.
Ikiwa kutakuwa na mvutano kidogo huo ndio mkutano wenyewe haitakuwa na maana kila kitu ambacho kinajadiliwa jibu inakuwa ni ndio.
Haijawahi kutokea hivyo mwanadamu mawazo yote yakwa sawa bila kupingana hapo kutakuwa na tatizo ni lazima mvutano wa hoja uwepo maisha yaendelee na mwisho muafaka upatikane.
Ipo wazi kuwa hata wafanyabiashara nao hufanya hivyo ikiwa bidhaa ambayo inaingia sokoni itajadiliwa kwa ubora wake haitaboreshwa na badala yake kuna vitu vinaweza kupunguzwa.
Jambo la msingi mapungufu yajadiliwe kisha yafanyiwe kazi maisha yaendelee.
Kila la kheri Wanachama wa Yanga na viongozi kwenye mkutano wenu wa leo ukawe ni mwendelezo wa mazuri kwa ajili ya manufaa ya mpira wetu.