THANK YOU KAKOLANYA

BENI Kakolanya kipa wa Simba anaingia kwenye orodha ya nyota ambao watakuwa kwenye changamoto mpya msimu ujao.

Kipa huyo aliibuka ndani ya Simba akitokea kikosi cha Yanga ilichokuwa kinanolewa na Mwinyi Zahera.

Ndani ya Yanga Kakolanya alifanya kazi kubwa ikiwa ni kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi alipookoa hatari zaidi ya 7 na kuliweka lango salama.

Taarifa kutoka Simba zimeeleza:”Uongozi wa klabu unaujulisha umma kuwa hatutaendelea kuwa na mlinda mlango, Beno Kakolanya baada ya mkataba wake kumalizika,”.

Nyota huyo kwenye mzunguko wa pili ndani ya kikosi cha Simba hakuwa akipewa nafasi zaidi ya kumshuhudia Ally Salim akifanya kazi kwenye lango la Simba licha ya kuwa ni kipa namba tatu.