>

DODOMA JIJI YAIPIGIA HESABU RUVU SHOOTING

UONGOZI wa Dodoma Jiji  FC umeweka wazi kuwa  mchezo wao wa mwisho dhidi ya Ruvu Shooting  unaotarajiwa kupigwa Juni  9 Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro wataingia kwa tahadhari kuwakabili.

Timu hiyo imekusanya pointi 34 baada ya kucheza mechi 29 nafasi ya 10 vinara ni Yanga wenye pointi 74 kibindoni.

Yanga wao kete yao ya mwisho itakuwa dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema hawaibezi Ruvu Shooting bali wanachukua tahadhari zote kuwakabili katika mchezo wao ujao.

“Ruvu Shooting ni  timu nzuri ina wachezaji wazuri , huwezi kuwabeza kwamba ni timu iliyoshuka daraja, kwa kuwa tunatambua ugumu na uzuri wa Ruvu Shooting ,kwahiyo tunajipanga  kukabiliana nao  katika mchezo wetu wa mwisho wakufunga msimu huu wa 2022/23.

“Msimu haukuwa mzuri kwa upande wetu,lakini kwa sasa akili na mipango yetu tunaielekeza zaidi katika mechi iliyopo mbele yetu ,ambayo tumepanga kuhakikisha alama tatu zinabaki kwetu baada ya hapo tutaanza maandalizi ya msimu ujao,” alisema Mpunga.

Mchezo wake uliochezwa Uwanja wa Majaliwa ulipata ushindi wa bao 0-1 dhidi ya Namungo ikiwa ugenini.