NYOTA wa Azam FC, Abdul Suleiman Sopu anatarajiwa kurejea kwa mara nyingine tena ndani ya Tanga, Uwanja wa Mkwakwani kupambania uzi wa timu yake dhidi ya Yanga.
Sopu aliibuka ndani ya Azam FC akitokea Coastal Union na kwa sasa yupo zake ndani ya Azam FC akipambania majukumu yake.
Azam FC itapambana na Yanga kwenye mchezo wa Azam Sports Federation ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Juni 12,2023.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 9:00 alasiri bingwa mpya atapatikana.