YANGA MATUMAINI YAKUTOSHA KIMATAIFA

NASREDDINE Nabi Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ado mchezo haujaisha kwenye anga la kimataifa licha ya kupoteza kweye fainali ya kwanza.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa umesoma Yanga 1-2 USM Alger ya Algeria.

Bao pekee la Yanga limefungwa na Fiston Mayele ambaye anafikisha jumla ya mabao 7 kwenye anga za kimataifa.

Kwa upande wa USM Alger walianza kupachika bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Mahlous na Merili aliyefunga kipindi cha pili.

Huu ni mchezo wa kwanza ikiwa ni fainali ambayo imechezwa Dar mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Juni 3,2023.

Kwenye mchezo wa leo imeripotiwa kuwa mashabiki 30 wamepata majeruhi huku mmoja ambaye ni mwanaume mwenye umri takriban miaka 40 ametangulia mbele za haki ikiwa ni taarifa za awali.