Home Sports HAPA NDIPO SIMBA ILIPOTUSUA

HAPA NDIPO SIMBA ILIPOTUSUA

WAKIWA mashuhuda wa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ukielekea kwa watani zao wa jadi Yanga, Simba wametusua katika vigongo vitatu vizito.

Yanga imetwaa ubingwa wa ligi ikiwa na pointi 74 baada ya kucheza mechi 28 wawa na Simba yenye pointi 67.

Ni safu ya ushambuliaji iliyofunga mabao mengi katika hili mastaa wa Simba walipambana kupachika mabao mengi ambayo ni 66.

Ikumbukwe kwamba ni Mtibwa Sugar imetunguliwa mabao mengi ambayo ni 44 ikiwa na pointi 29 kibindoni.

Kigongo kingine cha pili Kwa Simba kutusua ni kuwa timu iliyopoteza mechi chache ikiwa imefungwa mchezo mmoja ilikuwa dhidi ya Azam FC.

Ni Ruvu Shooting ya Pwani imepoteza mechi nyingi ambazo ni 18 ikiwa imeshuka daraja itashiriki Championship msimu ujao.

Kigongo cha tatu ilipotusua ni staa wake Clatous Chama kuwa namba moja kwa pasi za mwisho ndani ya ligi ambazo ni 14 na mbali na pasi hizo Chama kafunga mabao manne msimu wa 2022/23.

Previous articleUSM ALGER:HATUCHEZI NA MAYELE SISI
Next articleYANGA MATUMAINI YAKUTOSHA KIMATAIFA