YANGA YATAMBA KUMALIZA KAZI KWA MKAPA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mchezo wa ugenini wataumaliza kwa mpango mkubwa ili kazi ya kutinga hatua ya nusu fainali kimataifa.

Yanga ilishuhudia ubao ukisoma Rivers United 0-2 Yanga katika hatua ya robo fainali ya kwanza na mchezo wa pili unatarajiwa kuchezwa Aprili 30,Uwanja wa Mkapa.

Kwenye mchezo huo mabao yalifungwa na Fiston Mayele dakika ya 71 na 82 akitumia pasi za nahodha Bakari Mwamnyeto ambaye ni beki.

 Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa ni muhimu kupata ushindi kwenye mechi zote mbili ili wafanikishe malengo ya kutinga hatua ya nusu fainali.

“Wananchi wanapenda kuona timu yao inashinda mechi zote mbili na inawezekana kutokana na uimara wa kikosi pamoja na mbinu za benchi la ufundi hivyo tumeanza ugenini kiasha kazi inamaliziwa Uwanja wa Mkapa.

“Tunahitaji kuandika historia nyingine kwenye anga la kimataifa hasa kwa wakati huu, walikuwa wanatubeza na kufikiria kazi imekwisha kwetu bado nguvu ni kubwa kwenye kusaka ushindi,” amesema Kamwe.