Home Sports MWAMBA WA KAZI NDANI YA SIMBA KAPOMBE HUYU HAPA

MWAMBA WA KAZI NDANI YA SIMBA KAPOMBE HUYU HAPA

MWAMBA huyu hapa ndani ya kikosi cha Simba uhakika kikosi cha kwanza kutokana na uwezo wa kupandisha mashambulizi na ana uwezo wa kufunga.

Mechi 21 dakika 1,866 mabao 2 pasi za mabao 6. Ikumbukwe kwamba alikosekana kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga. Tunakupitisha kwenye kazi zake ngumu ndani ya ligi msimu wa 2022/23.

Kutoka Morogoro,Tanzania ilipo ile milima ya Uluguru mshikaji anatokeo hapo anaitwa Shomari Kapombe kinara kwenye kutengeneza mipango kwa upande wa mabeki.

Mzawa mwenye juhudi ambaye uwezo wake unampa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kinachonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira.

Majanga

Msimu ulipoanza hakuwa fiti baada ya kupata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Mkapa Agosti 20,2022 aliposepa na dakika 66.

Baada ya hapo alikuwa anapambania hali yake na nafasi yake ilichukuliwa na Israel Mwenda akaibuka Septemba 14,2022 kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine aliposepa na dakika 90.

Bado hakuwa fiti kwa mara nyingine tena alikosekana mchezo wa Kariakoo Dabi 23,2022 na aliwakosa Azam pia Oktoba 27 Uwanja wa Mkapa.

Ngoma iliibuka tena Oktoba 30 walipovaana na Mtibwa Sugar aliposepa na daika 90 mazima hapo akawa imara zaidi na mpaka sasa anaendelea kupambana.

Baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar,Kapombe alisema kuwa:”Nimerejea kwa sasa nilikuwa ninapitia maumivu makubwa kwa kuwa ugonjwa ambao nilikuwa ninaumwa wakati mwingine nilikuwa ninaambiwa hawaoni ugonjwa.

“Lakini kwa sasa nimerejea kwenye ubora wa asilimia 100 nina mshukuru Mungu kwa haya yote, mashabiki wazidi kuwa pamoja,”.

Pasi zake

Ametoa pasi sita za mabao ndani ya ligi akiwa ni kinara kwenye upande wa watengeneza mipango wale wanaocheza nafasi ya beki kwenye ligi.

Pasi yake ya kwanza alitoa Uwanja wa Ushirika,Moshi mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ilikuwa dakika ya 38 akitumia mguu wake wa kulia Novemba 27,2022.

Pasi ya pili ilidondoka pale Uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Geita Gold ilikuwa dakika ya 11, Desemba 18,2022 kwa mguu wake uleule wa kulia.

Pasi ya tatu ilikuwa Uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya KMC dakika ya 15 ilikuwa Desemba 26,2022 mguu wa kulia.

Nne pasi yake ilikuwa mchezo dhidi ya Singida Big Stars dakika ya 63 Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Februari 3,2023.

Ngoma ya tano iligotea kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu alimpa mshikaji wake Jean Baleke dakika ya 33 kwa pigo la kichwa.

Ile ya sita ilikamilika kwenye mchezo dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 16ambapo ubao ulisoma Simba 2-0 Yanga ilikuwa dakika ya kwanza akitumia mguu wa kulia.

Bao kwenye mchezo huo lilipachikwa kimiani na beki Henock Inonga hivyo kazi ya beki ilimalizwa na beki.

Bao lake la kwanza aliwatungua Tanzania Prisons ilikuwa Uwanja wa Mkapa kwa pigo la kichwa ngoma ilichezwa Desemba 30,2022.

Akawatungua Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa dakika ya 35 kwa mguu wake wa kulia ilikuwa ni 19/11/2022.

Mshikaji wake Mohamed Hussein anafuatia kwa mabeki wenye pasi nyingi kibindoni akiwa nazo tano ndani ya ligi na wote wapo ndani ya Simba.

Imeandikwa na Dizo Click kutoka gazeti la Championi.

Previous articleAZAM FC KUSUKA KIKOSI CHA KAZI KUIMALIZA SIMBA
Next articleYANGA YATAMBA KUMALIZA KAZI KWA MKAPA