KALI Ongala, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa watapata muda wa kuunda mpango kazi kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi ijayo dhidi ya Simba.
Timu hiyo inatarajiwa kumenyana na Simba mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la Azam Sports Federation, Uwanja wa Nangwanda ambapo bingwa mtetezi ni Yanga.
Yanga wao watacheza hatua ya nusu fainali na Singida Big Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Liti, Singida.
Ni Mei 6 mchezo huo unatarajiwa na mshindi atamenyana na atakayepenya kwenye mchezo kati ya Singida Big Stars ama Yanga watakaocheza nusu fainali Uwanja wa Liti.
Ongala alisema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wanatambua mchezo ujao dhidi ya Simba watafanya kazi kubwa kwa ajili ya kupata matokeo.
Mchezo wao uliopita wa ligi ubao wa Uwanja wa Jamhuri,Moro ulisoma Ruvu Shooting1-3 Azam huku Ayoub Lyanga akitupia mabao mawili na moja mali ya Sopu.
“Tuna mchezo mgumu dhidi ya Simba ambao wote tutakuwa ugenini hivyo tunakwenda kukutana na ushindani mkubwa kutoka kwa mpinzani ambaye anahitaji matokeo chanya.
“Muda ambao tunao tutatumia kuandaa kikosi kwa ajili ya kupata ushindi na hilo linawezekana hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja kuelekea mchezo wetu,”.
Leo Aprili 30 Azam FC inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC Uwanja wa Azam Complex.