KIPA SIMBA AWEKA REKODI YAKE MATATA

ALLY Salim kipa namba tatu wa Simba ameonesha uimara wake akiwa langoni ndani ya dakika 270 kwa kuyeyusha dakika zote hizo bila kutunguliwa hata walipokutana na watani zao wa jadi Yanga.

Nyota huyo alipewa mikoba ya kipa namba moja wa Simba Aishi Manula na ile ya kipa namba mbili Beno Kakolanya kwenye mechi tatu mfululizo.

Kete yake ya kwanza kwa msimu wa 2022/23 kukaa langoni ilikuwa dhidi ya Ihefu huu ulikuwa mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya Manula kupata maumivu kwenye mchezo dhidi Ihefu uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Manula kwenye mchezo huo alimpisha Kakolanya ilikuwa dakika ya 75 ilikuwa ni Aprili 7, kilichofuata kwenye mechi tatu ni Salim alikaa langoni.

Ilikuwa ni Aprili 10,2022 ubao wa Highland Estate ulisoma Ihefu 0-2 Simba, kipa huo aliokoa michomo ya Yacouba Songne, Adam Adam ambao walikuwa kwenye safu ya ushambuliaji.

Ngoma ikapigwa tena kwenye Kariakoo Dabi, Aprili 16, Simba 2-0 Yanga, mbele ya Fiston Mayele mshambuliaji namba moja Bongo mwenye mabao 16 na pasi moja pamoja na Kennedy Musonda kijana alitimiza majukumu yake.

Kwa mara ya kwanza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni dhidi ya Wydad Casablanca mabingwa watetezi wa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika alisepa na dakika 90 huku akitimiza majukumu yake kwenye kuweka lango salama.

Ukuta wa Simba chini ya Joash Onyango, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe na Henock Inonga ulitimza majukumu kwa umakini na kufanikisha malego ya timu kupata ushindi.

Roberto Oliveira amesema kuwa kila mchezaji ni muhimu kupata nafasi kikosi cha kwanza kutokana na uwezo wake.

“Tuna wachezaji wengi Simba wenye uwezo mkubwa ninafurahia kuona wanaonyesha kile ambacho wanakifanya kwenye mazoezi, bado kuna kazi kubwa ya kufanya na watapata nafasi zaidi kwenye mechi zijazo,” .