JASHO LILIWAVUJA SIMBA DHIDI YA WYDAD

    ILIKUWA roho ya mnyama kwenye ardhi ya Bongo wakati wakipambana na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Wydad Casablanca.

    Weka kando kutokuwepo kwa kipa namba moja Aishi Manula kutokana na kutokuwa fiti bado ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-0 Wydad Casablanca.

    Kazi haijaisha ugenini hatma ya Simba itajulikana ila hapa tunakudondoshea namna wapambanaji walivyokuwa kwenye kazikazi namna hii:-

    Ally Salim

    Aliokoa hatari dakika ya 9,22,23,27,39,57,87,90 alipiga pasi ndefu dakika ya 3,33,77 zile pasi fupi ilikuwa dakika ya 20,57,87.

    Shomari

    Shomari Kapombe alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 69 alipewa majukumua kurusha dakika ya kwanza 7,37,54 huku akiokoa hatari dakika ya 16,48,59,78.

    Joash Onyango

    Kakamilisha dakika 90 bila kusababisha penalti katika mchezo dhidi ya Wydad na alivuja jasho akiokoa hatari dakika ya 23,38,58,67,87 na alionyeshwa kadi moja ya njano.

    Inonga

    Henock Inonga aliokoa hatari dakika ya 2,15,23,53,60,72,73 alipga faulo dakika ya 11,

    Mohamed Hussein Zimbwe Jr

    Aliokoa hatari dakika ya 49 alipiga krosi dakika ya 19,79 alipewa jukumu la kurusha dakika ya 38,64.

    Kibu

    Kibu Dennis kiungo wa Simba alichezewa faulo dakika ya kwanza, 3,10,18,83 alicheza faulo dakika ya 8,17 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 34,74 aliokoa hatari dakika ya 49.

    Mzamiru

    Mzamiru Yassin alichezewa faulo dakika ya 51 alirusha dakika ya 73 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 14.

    Chama

    Clatous Chama alicheza faulo dakika ya 42,90, alipiga faulo dakika ya 3,29 alipiga kona dakika ya 35 alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 46.

    Kanoute

    Sadio Kanoute kiungo mkabaji wa Simba karejea uwanjani na kusepa na dakika zote 90 ni dakika ya 26 aliokoa hatari huku akitembeza mikato yake ya kimyakimya dakika ya 12 alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 31,38 alitembezewa mikato dakika ya 65,71.

    Ntibanzokiza

    Saido Ntibanzokiza alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango dakika ya 5,58,alipiga krosi dakika ya 37 alirusha dakika ya 7,alichezewa faulo dakika ya 65,71 licheza faulo dakika ya 12 alisepa na dakika 80 nafasi yake aliingia Pape Sakho aliyechezewa faulo dakika ya 82.

    Baleke

    Jean Baleke aliyeyusha dakika 88 nafasi yake alichukua nahodha John Bocco alifunga dakika ya 30 alichezewa faulo dakika ya 29,46,62.

    Youssef El Motie

    Alianza langoni na alitunguliwa bao moja huku akiokoa hatari dakika ya 55,67,79 alipiga pasi ndefu dakika ya 19,34,36,38,52,55,67,69,71,75,76.

    Jamal Daoudi

    Nyota huyu alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 52 aliokoa hatari dakika ya 65.

    Abduolatif

    Aliokoa hatari dakika 7 alionyeshwa kadi moja ya njano.

    Asen Zola

    Mwamba huyu alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 16 huku akiokoa dakika ya 18,20,64,84 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 86.

    Yahya Abdalah

    Aliokoa hatari dakika ya 48,60 alicheza faulo dakika ya 45 alipiga kona dakika ya 23,38,48.

    Imeandikwa na Dizo Click.

    Previous articleBEKI YANGA AWEKA REKODI YAKE KIMATAIFA
    Next articleShangwe Kubwa La Bodaboda Lasababishwa Na Meridianbet