HAIWEZI kuwa kazi nyepesi kwa kuwa lazima mapambano yawe makubwa katika kufanya hilo jambo ambalo unalihitaji kwa wakati.
Kila mmoja kwenye Ligi Kuu Bara kwa sasa anapambana kuweza kufikia malengo ambayo alianza nayo mwanzo wa msimu wa 2022/23 ambao unakaribia kugota mwisho.
Hakika ni moja ya msimu wenye ushindani mkubwa na kila timu inafanya vizuri kwenye mechi zake ambazo inacheza hilo ni jambo kubwa na linapaswa kupewa pongezi.
Wale ambao wanashindwa kupata matokeo ni muda wao sasa kutazama kile ambacho kinawafanya washindwe kupata ushindi kwani hakuna shabiki ambaye anapenda kuona timu yake inashindwa.
Sio shabiki tu hata wachezaji nao furaha yao ipo kwenye ushindi jambo ambalo litawafanya waweze kutimiza malengo yao ambayo wanayo.
Hapa ni ngumu kuweza kuona timu inashindwa kupata matokeo ikiwa haitafanya maandalizi mazuri na ikishindwa kupata pia haina maana haikufanya maandalizi bali makossa ambayo iliyafanya.
Mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa hivyo ukikosea kwenye maandalizi utakosea kwenye mchezo husika wa kusaka pointi tatu muhimu.
Zipo timu ambazo zimekuw hazipati matokeo mazuri kwenye mechi ambazo wanacheza hiyo inatokana na ushindani mkubwa.
Hakika hili ni kubwa na linastahili pongezi kwa kila mmoja kufanya kile ambacho anahitaji na mwisho ni muhimu kupata matokeo mazuri.
Zile ambazo zimekuwa kwenye mwendo mbaya wa kukwama kupata matokeo ni muda wa kufanya kazi kubwa na kuongeza juhudi kwenye mechi ambazo zimebaki.
Baada ya dakika 90 na matokeo ambayo yanapatikana ni muhimu kujipanga kwa ajili ya mechi zilizobaki kwa hali na mali.
Kuwa kwenye ligi ni jambo moja na kushuka kwenye ligi ni jamo lingine pia hivyo kuna umuhimu wa kuweza kufanya hesabu zao mapema kabla ligi haijaisha.
Kwa mechi ambazo zimebaki na kwa tofauti ya pointi ambayo ipo kuna uwezekano wa kumaliza kwenye nafasi tofauti na waliyopo kwa sasa.
Lakini kinachotakiwa ni kujitoa kwa hali na mali kwa kuwa kila timu pale ambapo ipo haipo tayari kuona kwamba inatoka na kushuka daraja.
Mwendo wa Championship unajulikana namna ulivyo hasa ukizingatia kwamba kila mmoja anapambana huko kurudi ndani ya Ligi Kuu Bara.
Muhimu sana kufanya maandalizi na jambo ambalo linaishi kwa timu hizi kwa sasa lazima liweze kutafutiwa ufumbuzi.
Haina maana kwamba hazipambani kwa umakini hapana lakini kuwa kwenye mstari mwekundu kwa wakati huu wa lala salama ni alama nyekundu pia kwa timu hizo hasa zikikubali kile ambacho zinakipata.
Nina amini kwamba hizi timu zote zina wachezaji wazuri wenye uwezo wa kufanya vizuri kwenye mechi za ushindani hivyo ni muda wa kujipanga katika mechi hizi za mwisho.
Mwisho unakuja kwa namna yoyote muhimu kila timu kupambana kupata kile wanachostahili uwanjani.